Thursday, May 09, 2013

JORDAN KUSISHITAKI IRAEL BARAZA LA USALAMA

Serikali ya Jordan imetangaza azma yake ya kuushtaki utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo utaendeleza uchokozi na uvamizi dhidi ya Masjidul Aqswa. Abdullah  Ensour  Waziri Mkuu wa Jordan ameonya kuwa, uvamizi wa mara kwa mara unaofanywa na walowezi wenye misimamo ya kufurutu ada wa Kizayuni dhidi ya Masjidul Aqswa, unaonyesha kuwepo  njama chafu zilizopangwa na walowezi hao, lakini kwamba  serikali ya Amman haitavumilia vitendo hivyo. Wakati huohuo, wabunge wa Bunge la Jordan leo wameitaka serikali ya nchi hiyo kumtimua balozi wa Israel nchini humo sanjari na kumrejesha nyumbani balozi wa nchi hiyo aliyeko Tel Aviv. Hatua hiyo ya wabunge inatokana na kitendo kilichofanywa jana  na walowezi wa Kizayuni wakishirikiana na viongozi wa ngazi za juu wa chama cha Likud cha kushambulia Masjidul  al Aqswa na kufunga milango ya msikiti huo, ili  kuwazuia waumini wa Kiislamu kutekeleza ibada zao humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO