Kundi la Ikhwanul Muslimin la Jordan limetaka kufukuzwa balozi wa utawala wa Kizayuni huko Amman. Ikhwanul Muslimin ya Jordan imetoa taarifa na kuitaka serikali ya Jordan kumfukuza mara moja balozi wa utawala wa Kizayuni nchini humo kutokana na mashambulizi yaliyofanywa hivi karibuni na Israel katika msikiti wa al Aqswa. Taarifa ya Ikhwanul Muslimin ya Jordan imeongeza kuwa, serikali ya Amman ni mhusika wa udhaifu uliopo unaopelekea kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu katika ardhi za Palestina na kwamba mashambulizi katika msikiti wa al Aqsa ni njama za Wazayuni ambazo haziwezi kunyamaziwa kimya. Wakati huo huo wawakilishi wa bunge la Jordan wamesisitiza kwa kura nyingi kufukuzwa balozi wa utawala wa Kizayuni mjini Amman sambamba na kumuita nyumbani balozi wa nchi hiyo aliyeko Tel Aviv. Wabunge wa Jordan pia wamemuandikia barua Spika wa Bunge la nchi hiyo wakitaka kuangaliwa upya makubaliano ya amani ya "Wadi Araba" yaliyosainiwa kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO