Wednesday, May 15, 2013

KILA KATIKA WATU KUMI MMOJA NI MUATHIRIKA WA UKIMWI A/KUSINI

Mmoja  kati  ya  watu  kumi  nchini  Afrika  kusini ana virusi  vya  HIV, lakini  vifo  vinavyotokana  na  ukimwi  vinapungua  wakati  matibabu yanaanza  kuonekana  kuleta  tija. Afisa  wa  shirika  la  takwimu nchini  humo  alisema jana  kuwa  baada  ya  miaka  kadha  ya kuburuza  miguu   kuhusu  mzozo  wa  HIV  na  ukimwi tangu  mwaka 2004, Afrika  kusini  imetengeneza mpango  mkubwa  kabisa  wa matibabu  ya HIV. Ugonjwa  huo  utahusika  na  asilimia  32  ya  vifo mwaka  huu.  Licha  ya  kwamba  kiwango  hicho  ni  cha  juu, lakini ni upunguaji  wa  asilimia  48  kutoka viwango vya  mwaka  2005. Kiwango  cha   wastani  cha   maisha  kimepanda   hadi  miaka  59.6 kutoka  miaka  51.6 katika  mwaka  2005. Lakini  kiwango  cha matatizo  ni  kikubwa, ambapo  watu  wapatao  milioni  5.3 wanaishi na  na  virusi  vya  HIV  kutoka  idadi  ya  wakaazi  milioni  53  nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO