Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepanga kujenga bwawa litakalokuwa kubwa zaidi duniani itakapofika mwaka 2015. Taarifa zinasema kuwa, bwawa hilo lilikuwa lijengwe miaka kadhaa iliyopita, lakini ilishindikana kutokana na ukosefu wa fedha za kugharamia ujenzi huo. Taarifa zinasema kuwa, bwawa hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme ambao utaweza kudhamini nusu ya mahitajio ya bara la Afrika. Imeelezwa kuwa, bwawa hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 40,000 za umeme kwa saa. Taarifa kutoka Kinshasa zinasema kuwa, nusu ya uzalishaji wa umeme huo utapelekwa nchini Afrika Kusini, kwa vile nchi hiyo ndio mdhamini mkubwa wa ujenzi wa bwawa hilo, na umeme uliosalia utatumika ndani ya ardhi ya Kongo na nchi nyingine za ukanda wa Maziwa Mkuu ya Afrika.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO