Monday, May 20, 2013

WAZIRI MKUU WA CHINA AZURU INDIA


Waziri mkuu wa China, Li Keqiang ameanza ziara ya kihistoria nchini India, ziara inayolenga kujaribu kutafuta suluhu ya kimipaka ambayo imeibuka hivi karibuni baina ya mataifa hayo mawili. Ziara hii inakuja ikiwa yamepita majuma kadhaa toka kushuhudiwa makabiliano kati ya wanajeshi wa India na China kwenye eneo la mpaka wa Kashimir Mashariki mwa nchi hiyo.
Li Keqiang amekuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, waziri mkuu, Manmohan Singh mazungumzo ambayo mbali na kujadili suala la usalama kwenye eneo la milima ya Himalaya, pia wamejadili uhusiano wa kibisahara kati ya mataifa hayo mawili.Baadhi ya wanaharakati nchini India wamekosoa ziara hiyo kwa kile walichodai ni serikali ya India kushindwa kuweka sheria kudhibiti uwekezaji unaofanywa na raia wa China ambao wanachukua ajira za wenyeji pamoja na kugombea eneo la mpaka wake.
Waziri mkuu,Li Keqiang mbali na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Manmohan Singh, atakutana na waziri wa mambo ya nje wa India Salman Khurshid, na viongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini India cha BJP.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO