Saturday, May 18, 2013

MASHAMBULIZI DHIDI YA BOKO HARAM 3O WAUAWAWA

Serikali ya Nigeria imefanya mashambulizi ya kutokea angani katika kambi za wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Msemaji wa wizara ya ulinzi ameliambia shirika la habari la AFP kuwa takribani watu 30 wameuawa katika mashambulizi hayo yaliyofanywa jana na ndege za kivita. Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika mikoa mitatu ya Adamawa, Borno na Yobe siku ya Jumanne. Jeshi la Nigeria limefanya mashambulizi hayo ili kuwatimua wafuasi wa kundi la Boko Haram, kutoka kaskazini mwa nchi hiyo. Boko Haram limefanya msururu wa mashambulizi nchini Nigeria tangu mwaka wa 2009. Mgogoro huo umesababisha vifo vya takriban watu 3,600.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO