Wednesday, May 22, 2013

MISRI YASEMA WALIOTEKWA NYARA WAACHIWA HURU

Msemaji wa Jeshi la Misri, Ahmed Ali amesema kuwa maafisa 6 wa polisi pamoja na askari mmoja wa kulinda mpaka waliolekwa nyara wiki iliyopita katika eneo la Sinai wameachiwa huru. Ali amesema serikali haijafanya mazungumzo na watekaji nyara ingawa duru za habari zimefichua kwamba, huenda serikali imekubali matakwa ya watekaji nyara hao ambao walikuwa wametaka wanamgambo wa Kibedui waachiliwe. Msemaji wa Jeshi la Misri pia amesema kuwa kivuko cha Rafah kilichokuwa kimefungwa baada ya utekaji nyara huo kimefunguliwa tena. Maafisa hao wa usalama walitekwa nyara wiki iliyopita wakiwa wanapiga doria katika miji ya Rafa na Al-Arish katika eneo la Sinai. Punde baada ya tukio hilo, serikali ilituma kikosi maalumu cha jeshi pamoja na ndege za kivita katika eneo hilo kwa lengo la kuwakomboa mateka hao.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO