Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imeunda makundi mawili tofauti ya majaji watakaosikiliza kesi dhidi ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na mtangazaji wa radio, Bw. Joshua Sang. Mahakama hiyo imesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha haki inatendeka. Majaji watakaosikiliza kesi za Ruto na Sang ni pamoja na Olga Herrera, Robert Fremr na Chile Eboe-Osuji. Kundi lingine la majaji litashughulikia kesi ya Rais Kenyatta. Majaji wamekiri kesi ya Kenya inakabiliwa na changamoto nyingi lakini wamesisitiza kuwa haki lazima itendeke kwa upande wa utetezi na ule wa mashtaka. Kesi ya Kenyatta inatarajiwa kuanza mwezi Julai huku ile ya Ruto ikitarajiwa kuanza baadaye mwaka huu. Juhudi za viongozi hao kutaka kesi zao ziakhirishwe zimegonga mwamba baada ya majaji kutupilia mbali ombi hilo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO