Thursday, May 09, 2013

NAM YAITAKA UN KUICHUKULIA HATUA ISRAEL

Jumuiya ya NAM imetoa taarifa ya kulaani shambulizi lililofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya kituo cha utafiti huko Syria na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya utawala huo ghasibu. NAM imesema kwenye taarifa hiyo kwamba kitendo cha Israel cha kuingia katika anga ya Syria na kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya kituo cha utafiti mjini Damascus ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa. NAM imesisitiza kuwa, Uhuru wa kujitawala wa Syria na heshima ya ardhi ya nchi hiyo imehujumiwa na kwa mantiki hiyo, Baraza la Usalama linapaswa kuchukua hatua kali dhidi ya Tel Aviv kwa mujibu wa sheria. Syria kwa upande wake imesema inafikiria jinsi ya kujibu shambulizi hilo na imeonya kwamba jibu lake kwa Israel litakua kali.   

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO