Idara ya ujasusi nchini Urusi imesema kuwa imemkamata mwanadiplomasia wa Marekani ambae inadaiwa kuwa ni mfanyakazi wa shirika la ujasusi la CIA akifanya juhudi za kuwaajiri raia wa nchi hiyo kusaidia katika ujasusi. Ryan Fogle , afisa wa tatu katika ubalozi wa Marekani mjini Moscow, alikuwa amebeba vifaa maalum vya kiufundi, maelezo maalum yaliyoandikwa pamoja na kiasi kikubwa cha fedha wakati alipokamatwa usiku wa jana. Idara ya ujasusi ya Urusi FSB imesema kuwa Fogle amekabidhiwa kwa maafisa wa ubalozi wa Marekani.
Licha ya kumalizika kwa vita baridi, Urusi na Marekani bado zinaendelea na operesheni za kijasusi ,kila upande.
Kukamatwa kwa Fogle , hata hivyo kunaonekana kuwa ni mwanadiplomasia wa kwanza wa Marekani kutuhumiwa kwa kosa la ujasusi katika kipindi cha karibu muongo mmoja na inaonekana kuwa hatua hiyo itaongeza hali ya uhusiano ambao tayari uko katika hali mbaya kati ya nchi hizo mbili.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO