Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amekanusha vikali kuwepo wapiganaji wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon kwenye mapigano yanayoendelea nchini Syria kati ya majeshi ya nchi hiyo na makundi ya kigaidi. Sergei Lavrov amesema kuwa, taarifa za kiintelijensia walizozipokea kutoka Damascus zinaeleza kwamba, wanamgambo wa Hizbullah wako nchini Syria kwa shabaha ya kulinda maeneo matakatifu ili yasishambuliwe na makundi ya kigaidi.
Hivi karibuni kumetolewa uvumi unaoelezea kuwepo wapiganaji wa Hizbullah kwenye mapigano yanayoendelea nchini humo, na idadi kubwa ya wapiganaji hao wameuawa.
Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Hizbullah alisisitiza siku cache zilizopita kwamba wapiganaji wa Hizbullah wako nchini Syria kwa shabaha ya kulinda maeneo matakatifu, ikiwemo Haram ya Bibi Zainab AS mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) iliyoko mjini Damascus.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO