Monday, May 20, 2013

WAPIGANAJI 23 WA HIZBULLAH WAUAWA SYRIA


Jeshi la Syria usiku wa kuamkia leo limetekeleza mashambulizi zaidi ya anga kwenye ngome kuu ya wapiganaji wa Syria mjini Qusary, siku moja toka rais Bashar al-Asada asisitize kutong'atuka madarakani. Takribani wapiganaji 23 wa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon wameuwawa wakati wakipigana sambamba na wanajeshi wa serikali ya Syria katika shambulio hilo, taarifa za taasisi ya uangalizi wa haki za binadamu nchini humo imearifu.
Upinzani umekosoa hatua ya mashambulizi hayo ambayo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa mji huo ni muhimu kwa utawala wa Asad kwa kuwa unapakana na Lebanon ambako wapiganaji wa Hezbollah wanausaidia utawala wake. Umoja wa nchi za Kiarabu umeitisha mkutano wa dharura Alhamisi ya wiki hii kujadili machafuko yanayoendelea nchini humo wakati huu ambapo nchi za Urusi na Umoja wa Mataifa zimekubaliana kuitisha mkutano wa kimataifa kujadili hali ya Syria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO