Saturday, June 08, 2013

AHARAMIA WAWAACHIA HURU WAFANYA KAZI WATANO

Duru za kiusalama nchini Nigeria zimetangaza habari ya kuachiliwa huru wafanyakazi watano wa meli ya mafuta, waliokuwa wametekwa nyara wiki mbili zilizopita. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu hao walioachiliwa huru, ni raia wa Pakistan. Vitendo vya uharamia wa baharini, vimeongezeka katika pwani ya nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika. Aidha vitendo hivyo, vimekuwa vikiyatia hasara kubwa mashirika mbalimbali yanayofanya kazi za usafirishaji mafuta katika eneo hilo. Itakumbukwa kuwa, tarehe 25 mwezi uliopita wa Mei, maharamia nchini Nigeria, waliishambulia meli ya mafuta ya nchi hiyo na kuwateka nyara wafanyakazi watano wa meli hiyo ambao ni raia wa Pakistan. Duru za usalama nchini humo, zimeongeza kuwa, watu hao, wameachiwa huru bila ya kupatwa na madhara yoyote.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO