Wakazi wa mji wa Al-Qusair nchini Syria, wameanza kurejea mjini humo, kufuatia kumalizika oparesheni za kuusafisha mji huo kutokana na uwepo wa makundi ya kigaidi. Aidha wakazi hao, wamekusanyika katika medani kuu ya mji huo na kutangaza shukrani zao kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na jeshi la Syria la kuukomboa mji huo muhimu wa kiistratijia. Wakati huo huo jeshi la Syria limetangaza kuwa, katika oparesheni za kuukomboa mji huo wa kistratijia, lilifanikiwa kuwatia mbaroni magaidi 913 wenye jinsia za nchi kadhaa za Kiarabu na za Magharibi, huku wengine wakiuawa na wengine kukimbilia maeneo mengine. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jeshi la Syria pia limefanikiwa kuzima njama ya magaidi hao waliokusudia kuharibu ofisi yao kuu ya oparesheni za kijeshi katika mji huo na kwamba, hadi sasa ofisi hiyo iko mikononi mwa jeshi la nchi hiyo. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, kushindwa vibaya makundi ya kigaidi na waungaji wao mkono huko Qusair nchini Syria, kutawalazimisha magaidi kuketi pamoja na serikali ya Damascus ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO