Tuesday, June 04, 2013

MAREKANI YACHUKIA MAFANIKIO YA JESHI LA SYRIA

Seneta wa chama cha upinzani cha Republicans nchini Marekani, John McCain ameelezea kuchukizwa kwake na  mafanikio ya jeshi la Syria dhidi ya makundi ya waasi yanayoungwa mkono na Washington na waitifaki wake.
McCain ameiambia kanali ya televisheni ya CBS kwamba serikali ya Rais Barack Obama inafaa kuingilia kati mara moja la sivyo, Rais Bashar al Assad atazima kabisa nguvu za waasi hao na kwamba hilo litakuwa pigo kubwa kwa ikulu ya White House.
Wiki iliyopita, seneta huyo aliingia kinyemela huko Syria na kukutana na viongozi wa makundi ya waasi wenye silaha, jambo lililodhihirisha wazi uhusiano uliopo kati ya Marekani na makundi hayo ya waasi.
Huku hayo yakijiri, habari zinasema kuwa jeshi la Syria limeendelea na oparesheni kali za kuwasaka waasi katika mji wa Qusayr na kwamba magaidi kadhaa wa kundi la Jabhat an-Nusra wameuawa.
Kwa upande mwingine waasi wa Syria wamejaribu kumuua  kamanda mmoja wa harakati ya Hizbullah kwa madai kwamba harakati hiyo inamsaidia Rais Bashar Asad. Watu wenye silaha wamefyatulia risasi gari la kamanda huyo ingawa hawakufanikiwa kumuua au hata kumjeruhi. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO