Habari kutoka China zinasema kuwa, kwa akali watu 119 wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mkasa wa moto katika kiwanda kimoja cha kuku kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Habari zaidi zinasema kuwa, wafanyakazi 300 walikuwa kwenye kiwanda hicho wakati moto ulipozuka na kusambaa kwa haraka. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ingawa mashuhuda wanasema walisikia mripuko mkubwa na huenda mripuko huo ulisababishwa na mchanganyiko wa kemikali au nguvu za umeme. Mikasa ya moto si jambo geni nchini China ingawa serikali imesema mkasa wa leo ni mbya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 12 iliyopita. Shughuli za uokoaji zinaendelea huku uchunguzi ukianzishwa ili kubaini chanzo cha mripuko huo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO