Makundi ya kisiasa nchini Afrika Kusini yameitaja Marekani kuwa mporaji wa maliasili na utajiri wa nchi za Kiafrika, na yamepinga safari inayotarajiwa kufanywa na Rais Barack Obama wa Marekani nchini humo siku chache zijazo. Muungano wa wafanya biashara nchini Afrika Kusini COSATU umewataka wafanyakazi nchini humo kufanya maandamano ya kupinga safari hiyo. Bongani Masuku katibu wa masuala ya kimataifa wa COSATU amesema kuwa, siasa za Marekani zimejikita zaidi katika kuzalisha na kukithirisha silaha za nyuklia na kusambaza silaha ulimwenguni, jambo ambalo linavuruga amani, uadilifu, demokrasia na haki za binadamu. Amesema kuwa, Marekani ina majeshi ya kutekeleza oparesheni maalumu katika nchi kadhaa ulimwengu, hatua ambayo imesababisha ghasia na machafuko kwenye nchi kadhaa ulimwenguni. Hivi karibuni, Muungano wa Mawakili wa Kiislamu nchini humo ulivitaka vyombo vya sheria nchini humo kumtia mbaroni Rais Obama atakapoingia nchini humo kwa tuhuma za kutenda jinai na ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi mbalimbali duniani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO