Ibrahim Ibrahim Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Afrika Kusini amesema kuwa, nchi hiyo imeshaanza kupeleka wanajeshi wake katika eneo lililogubikwa na machafuko la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo chini ya mwamvuli wa vikosi maalumu wa Umoja wa Mataifa vya kupambana na waasi nchini humo. Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Afrika Kusini ameongeza kuwa, jumla ya wanajeshi 1345 wa nchi hiyo watapelekwa nchini Kongo, chini ya mwamvuli wa vikosi maalumu vya Umoja wa Mataifa. Nchi za Tanzania na Malawi zimeshapeleka wanajeshi wake 3,000 katika mji wa Goma ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tokea mwezi Mei uliopita.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO