Thursday, July 11, 2013

16 WAHOFIWA KUFA KWA MAFURIKO

Mafuriko  yanayotokea  katika  maeneo  ya  milima  ya Himalaya  magharibi  mwa  China   yameharibu  madaraja , nyumba  na  kusababisha  maporomoko  ya  ardhi , na watu  19  wanahofiwa  kuwa  wamefariki  na  wengine kadha  hawajulikani  waliko, wakati  mvua  kubwa zinanyesha  katika  maeneo  kadha  ya  nchi  hiyo. Mafuriko katika  jimbo  la  magharibi  la  Sichuan  ni  mabaya  kabisa katika  muda  wa  miaka  50  iliyopita  katika  baadhi  ya maeneo, wakati   zaidi  ya  watu  100,000  wamelazimika kuyahama  makaazi  yao.
Kwa  mujibu  wa  wizara  ya  masuala  ya  jamii  nchini humo , kiasi  ya  watu  wapatao  milioni  1.6  wameathirika tangu  Jumapili  iliyopita  na  nyumba  elfu  kadha zimeharibiwa.
Kiasi  ya  watu  100 wamekufa  ama  hawajulikani  waliko. Wengi  waliofariki   katika  jimbo  la  Sichuan  ni  kutokana na  maporomoko  makubwa  ya  ardhi  ambayo  yametokea katika  eneo  la  kitalii  nje  ya  mji  wa Dujiangyan. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO