WAZIRI WA NISHATI |
Rais Francois Hollande wa Ufaransa amemfuta kazi Waziri wa Nishati na Mazingira kwa kukosoa sera za kiuchumi za serikali yake. Ofisi ya Rais Hollande imetangaza kuwa nafasi ya Delphine Batho ambaye ni waziri wa kwanza kuwahi kuachishwa kazi katika serikali ya Kisoshalisti ya Ufaransa imechukuliwa na Philippe Martin. Bi Delphine amefutwa kazi na Rais Hollande kwa kukosoa hadharani mipango ya kubana matumizi ya serikali ya Paris yenye lengo la kupunguza nakisi ya bajeti ya mwaka 2014.
Hii ni katika hali ambayo Wizara ya Fedha ya Ufaransa imetangaza mipango yake ya kutaka kushughulikia nakisi ya bajeti ijayo kwa kupunguza matumizi ya serikali ya dola bilioni 18, punguzo la kwanza la aina yake kuwahi kufanywa nchini Ufaransa tangu mwaka 1958. Mipango hiyo ya kupunguza matumizi ya serikali nchini Ufaransa iliilenga pia Wizara ya Nishati na Mazingira ya nchi hiyo ambayo ilikuwa ya waziri huyo aliyeachishwa kazi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO