Serikali na wananchi wa Bolovia wamelaani hatua ya Ufaransa na Ureno ya kukataa ndege ya rais wao, Evo Morales kutumia anga yao na kusema jambo hilo lilikuwa na lengo la kumvunjia heshima na kuhatarisha maisha yake. Rais Morales alikuwa akirudi nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa nishati nchini Russia. Ndege yake ililazimika kutua kwa dharura mjini Vienna, Ausria baada ya Ufaransa na Ureno kukataa ndege isipae katika anga yao. Nchi hizo zilidai kwamba uamuzi huo ulisababishwa na hitilafu za kiufundi lakini duru zimefichua kwamba Paris na Lisbon zilishuku huenda Rais Morales alikuwa ameandamana na afisa wa zamani wa CIA ya Marekani anayesakwa, Bw. Edward Snowden. Jasusi huyo wa zamani wa Marekani anasakwa na nchi yake baada ya kufichua kwamba CIA na mashirika mengine ya kijasusi ya Washington yamekuwa yakifanya ujasusi dhidi ya watu kote duniani wakiwemo wanadiplomasia kwa kusikiliza kwa siri mazungumzo yao ya simu na kudukua baruapepe zao. Jambo hilo limezusha hasira kote duniani huku Umoja wa Ulaya ukitishia kuvunja mikataba ya kibiashara na Marekani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO