Nchini Marekani waendesha mashtaka katika mahakama ya kijeshi wamekamilisha kesi yao dhidi ya mwanajeshi anayeshtakiwa kwa kuvujisha nyaraka za siri kwa tovuti ya Wikileaks. Katika uvujishaji mkubwa kabisa wa nyaraka za siri katika historia ya Marekani, kuruta wa ngazi ya kwanza Bradley Manning, anakabiliwa na madai 21, ikiwa ni pamoja na ujasusi, udanganyifu katika kompyuta na kusaidia adui. Manning anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha bila msamaha iwapo atapatikana na hatia. Afisa wa kupambana na ujasusi katika jeshi ametoa ushahidi wake jana katika kikao cha faragha katika mahakama hiyo ya jeshi kuhusu thamani ya taarifa zilizotolewa kwa adui ambazo Manning alizivujisha. Waendesha mashtaka wa jeshi wanamtambulisha Manning kuwa ni mtu aliyefanya kitendo hicho bila msaada wa mtu mwingine, na ambaye alikuwa akijigamba kuhusu uwezo wake wa udukuzi katika kompyuta. Wanadai kuwa kiburi kilimfanya Manning, mwenye umri wa miaka 25, kuchukua hatua hiyo ya kuvujisha taarifa za siri. Wakili wa Manning amesema kuwa mwanajeshi huyo anayeaminika kuvujisha taarifa hizo hatayadhuru maslahi ya Marekani kwa kuwa hayazitatumika kwa lolote.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO