Gazeti la Wall Street Journal la Marekani limefichua kwamba mpango wa kuiondoa madarakani serikali ya aliyekuwa rais wa Misri, Muhammad Mursi ulitayarishwa miezi kadhaa iliyopita kati ya makamanda wa jeshi la nchi hiyo na vinara wa kambi ya upinzani. Ripoti ya gazeti hilo imeashiria vikao vya mara kwa mara vya jeshi la Misri na vinara wa kambi ya upinzani na kwamba jeshi liliwahakikishia wapinzani kwamba, litaingilia kati kumuondoa madarakani Muhammad Mursi iwapo wapinzani wa serikali watafanikiwa kukusanya idadi kubwa ya wananchi mitaani.
Gazeti la Wall Street Journal limefichua kwamba, miongoni mwa waliokuwa wakihudhuria vikao hivyo ni pamoja na Muhammad el Baradei, Amru Mussa na Hamdin Sabahi. Limesema kuwa katika vikao hivyo kambi ya upinzani ilitaka kuhakikishiwa kwamba, jeshi litaingilia kati kumuondoa madarakani Mursi au la.
Maelfu ya wananchi wa Misri wanaendelea kufanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wakipinga hatua ya jeshi la nchi hiyo ya kumuondoa madarakani rais aliyekuwa amechagulwia na wananchi Muhammad Mursi mapema mwezi huu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO