Mkuu wa chama cha Kikristo cha uhuru cha Kitaifa cha huko Lebanon amesisitiza juu ya kuundwa serikali mpya nchini humo kwa kuishirikisha harakati ya Hizbullah. Michel Aoun ameshiria mchakato wa Tammam Salam Waziri Mkuu Mpya wa lebanon wa kuunda serikali mpya na kueleza kuwa chama chake hakitashiriki katika serikali mpya iwapo Hizbullah haitashirikishwa katika serikali hiyo. Amesema hiii ni kwa sababu Hizbullah ni sehemu muhimu sana ya jamii ya Lebanon. Michel Aoun amesisitiza juu ya udharura wa kuungana matabaka mbalimbali ya walebanon na kuongeza kuwa chama cha Uhuru cha Kitaifa cha Lebanon daima kinaiunga mkono harakati ya Hizbullah ya nchi hiyo. Naye Nabii Beri spika wa bunge la Lebanon amekosoa msimamoo wa mrengo wa Machi 14 na kueleza kuwa kundi lililokwamisha kuundwa serikali nchini humo si Hizbullah wala Amal bali ni mrengo huo wa Machi 14 ambao umekwamisha uuandaji wa serikali mpya kwa kutoa masharti yasiyokubalika likiwemo la kutaka kutengwa Hizbullah.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO