Katibu Mkuu wa Harakati ya al Wifaq nchini Bahrain amesema kuwa, kamwe harakati ya wananchi haitasimamishwa nchini humo na kusisitiza kuwa, wananchi wa Bahrain hawaogopi kusimama kidete kwenye mapambano yao dhidi ya utawala wa Aal Khalifa. Sheikh Ali Salman amesema kuwa, wanamapinduzi wanachunguza na kuangalia upya misimamo yao juu ya suala la kufanyika mazungumzo na utawala wa Aal Khalifa kwa shabaha ya kuikwamua nchi hiyo kwenye mgogoro na machafuko yanayoikabili hivi sasa. Sheikh Salman amesisitiza kuwa, harakati za wananchi hazitasimamishwa hadi pale yatakapotekelezwa matakwa ya wananchi wa Bahrain. Katibu Mkuu wa al Wifaq amebainisha kuwa, utawala wa Bahrain unapasa kuheshimu demokrasia sambamba na kuacha kuiendesha nchi hiyo kwa mkono wa chuma.
Wakati huohuo, wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano makubwa dhidi ya utawala wa nchi hiyo, na kusema kuwa Hamad bin Issa Aal Khalifa Mfalme wa Bahrain ndie mhusika mkuu wa ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya wanaharakati na raia wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO