Thursday, July 11, 2013

OIC YATAKA UN KUWASAIDIA WAISLAM WA MYANMAR

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua imara zaidi ili kuhitimisha dhulma wanayofanyiwa Waislamu nchini Myanmar. Hayo yamesemwa Jumatano katika mkutano baina ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mabalozi wa nchi za OIC katika umoja huo. Mabalozi hao kutoka nchi za Kiislamu duniani wametaka Umoja wa Mataifa uishinikize serikali ya Myanmar itatue matatizo yanayowakabili Waislamu wa kabila la Rohingya nchini humo.
Malefu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na maelfu ya wengine kuachwa bila kufuatia hujuma ya Mabuddha wenye misimamo mikali katika jimbo la Rakhine mashariki mwa Myanmar. Aidha Mabudhaa hao wanaopata himaya ya vikosi vya usalama wameteketeza moto misikiti na nyumba za Waislamu. Balozi wa Djibouti katika Umoja wa Mataifa Roble Olhaye ambaye pia ni mwenyekiti wa mabalozi wa OIC katika umoja huo ametaja hujuma dhidi ya Waislamu Myanmar kuwa ni mauaji ya umati.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO