Tuesday, July 16, 2013

RAJOY AKATAA KUJIUZULU

Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amepuuza wito unaomtaka kujiuzulu kutokana na kashfa inayoitikisa serikali yake. Ametupilia mbali shinikizo kutoka kwa wapinzani wake kisiasa ambao wanamtaka kuachia ngazi kutokana na tuhuma kuwa alipokea malipo ya siri kupitia chama chake alipokuwa waziri miaka ya 1990.
Rajoy amewaambia waandishi wa habari mjini Madrid kuwa atakamilisha majukumu aliyopewa na wapiga kura, na ataendeleza mapambano kujaribu kurejesha utengamano wa kiuchumi katika nchi yake inayokabiliwa na mdororo. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 58 amesema hakufanya kosa lolote.
Mweka hazina wa chama chake Luis Barcenas ambaye yuko jela kwa hatia ya kupokea rushwa alitoa ushahidi mahakamani akimshutumu Rajoy na maafisa wengine wa chama chake kupokea malipo yasio halali. Chama cha Rajoy, Popular Party kimekanusha kuwepo kwa malipo ya kichinichini.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO