Umoja wa Mataifa umesikitishwa na kupungua kwa vikosi vyake vya kulinda amani kwenye milima ya Golan na inafanya jitihada za kuajiri vikosi vingine kutoka Ulaya ili kuziba mwanya huo, Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon amesema jana Jumatatu. Kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa cha UNDOF kilichopo kwenye mpaka tete wa Syria na Israel kimeshuhudia idadi ya wanajeshi wake wakipungua na kufikia 530 kutoka 1050 baada ya Japana na Croatia kuondoa vikosi vyao.
Austria ambayo awali ilikuwa mchangiaji mkuu ,itaondoa wanajeshi wake kufikia mwishoni mwa mwezi huu huku kukiwa na hofu ya kuenea kwa ghasia dhidi ya walinda amani, na kuacha kikosi imara cha wanajeshi 530 kutoka Ufilipino na India. Ban amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi kuwa mamlaka ya UNDOF katika milima ya Golani ni muhimu sana kwa ajili ya kudumisha amani na usalama katika kanda, na si tu katika eneo hilo na kusisitiza kuwa amesikitishwa sana na kujiondoa kwa vikosi vya Austria.
UNDOF na wanachama wengine 76 wa makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya kusitisha mapigano, wanasimamia mkataba wa kusitisha mapigano uliosainiwa mwaka 1973 baada ya vita ya Yom Kippur, vita ambayo ilishuhudia Israeli ikuchukua sehemu ya eneo muhimu la milima ya Golani kutoka kwa maadui zao Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO