Saturday, July 06, 2013

VENEZUELA YAKUBALI KUMPA HIFADHI SNOWDEN

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amethibitisha uamuzi wa serikali yake kumpatia hifadhi ya kisiasa mfanyakazi wa zamani wa shirika la kijajusi la CIA Edward Snowden anayesakwa baada ya kuvujisha siri za ndani za Marekani. Maduro ameweka wazi uamuzi huo wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa Venezuela yaliyofanyika siku ya ijumaa ijumaa. Wakati huo huo Nicaragua kupitia kwa Rais wake Daniel Ortega nao wameidhinisha kumpa hifadhi Snowden ambaye anasadikiwa yupo katika uwanja wa ndege jijini Moscow toka alipowasili akitokea Hong Kong kwa takribani majuma mawili.
Snowden anayejitahidi kuepuka kuangukia mikononi mwa Marekani alituma maombi hayo kwa takribani 27, nchi nyingi za Ulaya zimekataa ombi hilo huku zile za Amerika Kusini ndizo zilizoonyesha nia ya kumpokea. Sakata la Snowden limeendelea kuzua utata katika siku za hivi karibuni wakatri huu ambapo Marekani imeendelea kuhaha kuhakikisha inamtia nguvuni ili akajibu mashtaka yanayomkabili baada ya kuvujisha siri za ndani za shirika la kijasusi la CIA.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO