Saturday, July 13, 2013

WAFANYAKAZI BRAZSIL WAANDAMANA NA KUFUNGA BARABARA

Wafanyakazi walioingia katika mgomo walifanya maandamano jana na kufunga Barabara kuu nchini Brazil Maandamano yaliyoitishwa na Vyama vya Wafanyakazi kudai mazingira mazuri ya kazi na kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kudhibiti kupanda kwa gharama za maisha. Maandamano haya yameitishwa na Vyama vikuu vitano vya Wanyakazi wakati wa Maandamano ya mwezi uliopita kudai huduma nzuri za jamii na kumaliza vitendo vya rushwa. Vyama vya Wafanyakazi wakidai mishahara bora, kupunguzwa kwa saa za kazi, usalama kazini na kuboreshwa kwa huduma za Afya na Elimu.
 Jijini Rio de Janeiro, Waandamanaji walijaribu kuvamia Jengo la Serikali lakini walitawanywa na Jeshi na Polisi kwa kutumia Gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira. Ingawa maandamano yalikuwa ya amani , giza lilipoingia Waandamanaji walianza kufanya vurugu kwa kuwashambulia polisi ambao waliwatawanya kwa Gesi ya kutoa machozi. Kutokana na Vurugu hizo maandamano yalisitishwa kabla ya kufika mwisho na Takriban Watu 12 walikamatwa na Polisi.
Mgomo wa wafanyakazi ulioambatana na maandamano yaliyogeuka ghasia uliandaliwa kwenye majimbo ishirini na sita nchini Brazil kitu ambacho kinaendeleza shinikizo kwa Serikali kuhakikisha inafanya mabadiliko ya sera zake.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO