Saturday, July 13, 2013

UN YAHOFIA USALAMA WA RAIA WA HOMS, SYRIA

Umoja wa mataifa umesema kuwa silaha za aina mbalimbali na vifaru vimeendelea kutumika katika mashambulizi yanayozidi kuwa mabaya siku hadi siku katika mji wa Homs nchini Syria jambo linalotishia usalama wa raia.
Mkuu wa shughuli za msaada wa kibinadamu wa umoja huo Valerie Amos na mkuu wa haki za binadanu Navi Pillay wametoa wito mpya wa kufikiwa kwa mji wa Homs lakini vikosi vya Rais Bashar al-Assad na waasi wa upinzaniwamekuwa wakikataa kuwapa uhakika juu ya usalama wao. Umoja wa Mataifa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) wamesema wako tayari kukimbiza misaada ya kibinadamu kama ingewezekana kuzuia mapigano.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO