Monday, July 08, 2013

WATU 40 HAWAJULIKANI WALIPO BAADA YA AJALI YA TRENI YA MAFUTA KUSHIKA MOTO

Maafisa wa usalama nchini Canada wamesema shughuli za kuwatafuta watu 40 ambao hawajulikani waliko, baada ya ajali treni ya mafuta kushika moto mwishoni mwa wiki iliyopita, imetatizika kutokana na mazingira magumu. Mkuu wa polisi wa eneo hilo la Quebec, Benoit Richard, amesema hakukuwa na shughuli ya uokozi jana usiku kwa sababu hali bado ni ya hatari mno, huku wazima moto wakijaribu kwanza kuhakikisha kuwa moto huo umezimwa kabisa. Richard amesema wengi wa wanaoshukiwa kutojulikana waliko walikuwa wanakunywa katika mkahawa mmoja karibu na ajali hiyo ilipotokea na mpaka sasa bado maafisa hao hawajaweza kufikia baa hiyo. Kiasi ya thuluthi moja ya idayi ya wakaazi 6,000 wa eneo hilo walilazimika kuhama makwao kutokana na moto huo uliosababishwa na ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO