Polisi nchini Uturuki wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji mjini Istanbul ambao wanataka Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan ajiuzulu. Jana Jumamosi waandamanaji walikusanyika katika medani ya Taksim wakijaribu kuingia katika Bustani ya Gezi ambayo imefungwa.
Ghasia Uturuki zilianza kufuatia mpango wa serikali wa kuharibu bustani ya Gezi na badala yake kujenga maduka. Bustani ya Gezi imezoeleka kuwa eneo la mijumuiko, mikusanyiko na maandamano na pia kivutio cha watalii huku ikiwa ni sehemu pekee ya kijani ya umma iliyobakia kwenye mji wa Istanbul. Mamia ya watu wamejeruhiwa na wengine wengi kutiwa mbaroni katika vurugu hizo. Waandamanaji aidha wamelaani vikali msimamo wa Erdogan wa kuunga mkono magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya wananchi wa Syria. Waturuki sasa wanataka Waziri Mkuu Erdogan ajiuzulu na kuitishwa uchaguzi wa mapema. Serikali ya Uturuki imesema kuwa huenda ikaitisha kura ya maoni kuhusiana na mpango wa kubomolewa bustani ya Gezi iliyoko karibu na medani ya Taksim mjini Istanbul ili kujaribu kumaliza maandamano ya kupinga serikali yanayoendelea nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO