Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali mlipuko wa kigaidi uliotokea jana mjini Beirut Lebanon na kusema Tehran inaungana na familia za wahanga wa tukio hilo katika maafa hayo. Sayyid Abbas Araqchi amesema wananchi wa Lebanon hususan harakati ya mapambano ya nchi hizo watashinda njama hiyo chafu ya Wazayuni na vibaraka wao ya kutaka kuzusha machafuko nchini humo. Umoja wa Mataifa na nchi mbalimbali duniani zimeendelea kulaani vikali mlipuko wa kutegwa ndani ya gari uliotokea jana jioni majira ya saa 12: 15 huko kusini mwa mji mkuu wa Bairut, Lebanon.
Katika mlipuko huo, watu 25 wameripotiwa kuuawa na wengine 200 kujeruhiwa sambamba na kuharibu nyumba magari yaliyokuwa karibu na eneo la tukio. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mlipuko huo na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga.
Nchi mbalimbali duniani ikiwemo Syria, Uturuki, nchi za Ulaya na kadhalika zimelaani vikali shambulizi hilo. Mlipuko huo wa kigaidi. Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas mbali na kulaani mripuko huo wa kusini mwa Bairut, imetaka kudumishwa umoja na mshikamano kati ya makundi yote ya Lebanon mbele ya njama za maadui.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO