Rais Barack Obama wa Marekani ametoa taarifa kuhusiana na hali nchini Misri baada ya jeshi nchini humo kuwaondoa kwa nguvu waandamanaji mjini Cairo jana. Obama amesema kuwa anasitisha ushirikiano wa kijeshi ambapo majeshi ya nchi hizo yalitarajiwa kufanya mazoezi ya pamoja mwezi huu. Pia Obama amesema Wamisri hawapaswi kuilaumu Marekani kwa kile kinachotokea nchini humo.
Wakati huo huo waandamanaji kutoka makundi ya Kiislamu nchini Misri wamevamia makao makuu ya gavana mjini Cairo leo na kuchoma moto jengo hilo. Kituo cha binafsi cha televisheni cha CBC kimeonesha picha za makao makuu hayo yakiwaka moto wakati wazima moto wakijaribu kuuzima moto huo.
Nao maafisa nchini Misri wamesema kuwa idadi ya watu waliouawa katika mapambano kati ya polisi na waandamanaji wanaomuunga mkono rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Mursi imefikia zaidi ya watu 525.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO