Mahakama Kuu ya Umoja wa Ulaya imepitisha uamuzi
wa kuondolewa vikwazo benki inayomilikiwa na serikali ya Iran ijulikanayo kama
Bank Saderat.
Katika uamuzi wake, mahakama hiyo imelitaka
Baraza la Ulaya kuiondoa Bank Saderat katika orodha ya benki zilizowekewa
vikwazo baada ya kusikiliza kesi iliyowasilishwa na benki hiyo.
Katika uamuzi wake, mahakama hiyo imesema vikwazo
dhidi ya Bank Saderat ni kinyume cha sheria. Wiki iliyopita pia Mahakama ya
Uadilifu ya Ulaya ilibatilisha vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya benki
nyingine ya Iran ijulikanayo kama Bank Mellat. Mwezi Desemba mwaka 2012 vile
vile mahakama hiyo ya Uadilifu ya Ulaya yenye makao yake Luxemburg iliuamuru
Umoja wa Ulaya ubatilishe vikwazo vyake dhidi ya benki nyingine ya Iran
ijulikanayo kam Sina Bank. Ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa mwaka 2012, Marekani na
Umoja za Ulaya ziliidhinisha vikwazo dhidi ya sekta za mafuta na za fedha za
Iran kwa lengo la kuzuia nchi zingine kununua mafuta ya Iran na kushirikiana na
Benki Kuu ya Iran. Marekani na waitifaki wake wameiwekea Iran vikwazo kwa madai
kuwa mpango wake wa kuzalisha nishati ya nyuklia una malengo ya kijeshi. Iran
imekanusha madai hayo na imeweza kuthibitisha kuwa miradi yake ya nyuklia
inafanyika kwa malengo ya amani na kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO