Thursday, October 08, 2015

8 tips for buying shoes that are good to your feet

Buying the right shoes is an investment in foot health. But how do you find ones that fit properly and provide adequate support? 
Start with your own feet, and look at what's already in your closet. Stand barefoot on a piece of paper or cardboard, and trace the shape of each foot. Now take your shoes, one by one, and place them on top of the drawing. If you're like most people, your "comfortable" shoes will closely match the outline of your own feet.



Identify the shoes that cause pain. If you're a woman, most of these will be shoes with narrow toes or high heels. Check to see if the toe of the shoe is narrower or shorter than your own toes.
When you're ready to replace some of that uncomfortable footwear, these tips can help:
  1. Wait until the afternoon to shop for shoes — your feet naturally expand with use during the day and may swell in hot weather.
  2. Wear the same type of socks that you intend to wear with the shoes.
  3. Have the salesperson measure both of your feet — and get measured every time you buy new shoes. If one foot is larger or wider than the other, buy a size that fits the larger foot.
  4. Stand in the shoes. Make sure you have at least a quarter- to a half-inch of space between your longest toe and the end of the shoe.
  5. Walk around in the shoes to determine how they feel. Is there enough room at the balls of the feet? Do the heels fit snugly, or do they pinch or slip off? Don't rationalize that the shoes just need to be "broken in" or that they'll stretch with time. Find shoes that fit from the start.
  6. Trust your own comfort level rather than a shoe's size or description. Sizes vary from one manufacturer to another. And no matter how comfortable an advertisement claims those shoes are, you're the real judge.
  7. Feel the inside of the shoes to see if they have any tags, seams, or other material that might irritate your feet or cause blisters.
  8. Turn the shoes over and examine the soles. Are they sturdy enough to provide protection from sharp objects? Do they provide any cushioning? Also, take the sole test as you walk around the shoe store: do the soles cushion against impact? Try to walk on hard surfaces as well as carpet to see how the shoes feel.

Vitamins and your heart

Do vitamin and mineral supplements really promote heart health? Some older studies suggested that calcium supplements have heart health benefits. Studies on fish oil showed it was is good for your heart, too. But calcium supplements have come under scrutiny following a report that men who took more than 1,000 milligrams of supplemental calcium daily over a 12-year period were 20% more likely to succumb to heart disease than those who didn't take the pills. And while some studies have found that popping fish oil capsules lowers the chance of having a heart attack or other related problem, others have failed to find such benefits.
Some observational studies have also shown links between heart health and higher intakes of certain vitamins — specifically, vitamins C and E, beta carotene, and three B vitamins (folic acid, B6, and B12). But more rigorous studies that compared people who took specific vitamins with those who took placebos have come up short. In fact, guidelines from the American Heart Association state that supplements of the vitamins listed above should not be taken to prevent heart disease. Not only do they not help, there's even some suggestion that taking vitamin E supplements may slightly raise the risk of heart failure and hemorrhagic (bleeding) strokes.
 Displaying

Sunday, March 08, 2015

MATOKEO YA FORM FOUR NA ALAMA ZAKE

Assalam alaikum warahmatullah.

Naomba nifikishe ktk kazi ile mlionipatia ya kuresearch abt distribution of grades na considerations zake;
A-Excellent
B plus-v. good
B- good
C-credit
D-pass
E-satisfactory
S-sabsi
F-failed
hivyo mtoto akiscore kuanzia A-D atakua amefaulu na ataweza kujiunga na A level na technical college kwa wale wenye A-C na vyuo uvya ualimu wa primary schools (diploma in primary education) kwa wale waliopata D plain ktk score zao.
Incase of GPA;
5-1.5 -wataweza kujiunga na A level and technical colleges including ile criteria ya grade point ya masomo husika aidha na combination or course
1.4-0.9 hawa wanaweza jiunga na diploma za ualimu wa elimu ya msingi na zile certificates wanazo tarajia wenyewe kufanya plus grade point za masomo husika yaani pass or satisfactory

Sent from my Windows Phone

Saturday, December 06, 2014

GOOGLE KUTOKA TANZANIA

Wakati nikifanya tafiti zangu za maswala ya shule na kujifunza mambo kadha wa kadha, nikajikuta natafiti juu ya mtandao mkubwa duniani ujulikanao kama "GOOGLE". Imekuwa ni jambo la kawaida kabisa na si la kushangaza kwa wengi pale unapotaja maswala ya kimtandao basi huwezi kukwepa kuutaja mtandao huu. Kwa hapa kwetu Tanzania naweza kuufananisha mtandao huu kama vile zilivyo bidhaa za Bakhresa kwa mkoa wa Dar es salam. Maana kila ukipita basi utakutana na maji, kama si maji basi biskuti, kitoroli cha "ice cream", mkate ama unga wa ngano wenye nembo ya bakhresa. Vile vile, unapokuwa mtandaoni basi ni nadra sana kuukimbia mtandao huu kwani unamiliki makampuni meng kwa wakati mmoja mfano mtandao wa video wa "youtube", google maps, gmail, google drive, google pictures na hata mtandao huu wa "blogspot" unaorahisisha watu kumiliki tovuti basi unamilikiwa na google. 
Mtandao huu umeleta mabadiliko makubwa duniani na bado unaendelea kuleta mafanikio miongoni mwa jamii ya dunia. Lilikuwa ni wazo la wanafunzi wawili tu wa chuo wakati wakisoma na leo ndio viongozi wakuu wa mtandao huu. 
Hivyo basi nirudi kwenye mada kuu, kutokana na mafanikio makubwa ya mtandao huu niliyoyaeleza hapo juu, nimepata kukutana na mawasiliano ya video yaliofanyika kutoka New York, Marekani mpaka katika shule ya msingi ya Katoke iliyopo biharamlo, Tanzania na watu kweza kushuhudia moja kwa moja sehemu nyingine kabisa. Waweza kuitazama video hiyo sasa kwa link hii video

Friday, July 11, 2014

MASHAMBULIZI YA WAISRAEL KATIKA MSIKITI WA AL-AQSA


Wakati waislamu wote duniani waiwa katika mfungo wa Ramadhani, Wapalestina na maeneo mengine yenye waislamu hayana furaha. Tunashuhudia kwa siku ya pili sasa mauaji ya wanawake na watoto yakiedelea huko Gaza nchini Palestina. Hii ni moja ya video zilizosambaa mitandaoni ikionesha mashambulizi katika msikiti wa Al-Aqsa, miongoni mwa maeneo matukufu kwa waislamu. Jeshi la Israel ndo linatekeleza mashambulizi hayo bila huruma wala aibu yoyote ile huku taasisi za umoja wa mataifa na tasisi za haki za binaadamu zikikaa kimya kabisa. Pia vyombo vya habari tunavyovijua vya kimataifa vimekuwa washabiki wa upande mmoja wa habari, vikionesha kama vile israel imekuwa ikionewa wakati huohuo havioneshi ni jinsi gani wapalestina wakiuwawa hasa wale wasiokuwa na hatia kabisa kwani mashambulizi yamekuwa yanafanyika katika makazi ya watu na sio katika maeneo ya kivita. Mungu Awafanyie wepesi watu wa Palestina na audhalilishe utawala haramu wa kizayuni. Ameen!!  

Thursday, July 03, 2014

WANASAYANSI WAGUNDUA UCHAPISHAJI WA MISHIPA YA DAMU

Ogezeko la maendeleo ya kiteknolojia yamepelekea watu kufikiri njia mbadala za kurahisisha maisha zaidi. Katika swala la afya, tunashuhudia ugunduzi mkubwa wa kitabubu ambapo wanasayansi kutoka maeneo mbalimbali duniani wantumia muda wao mwingi katika utafiti. Mpaka leo bado kuna uhaba wa viungo vya binaadamu ambapo watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na uhaba huu. Njia inayotumika mpaka sasa ni ya kupewa viungo mfano wa figo kutoka kwa mtu mwingine. Miaka ya karibuni, watu walizindua mashine za uchapishaji wa vitu halisi yaani "3D printing". Sasa teknolojia hiyo inaunganishwa na afya kwa ajili ya kuchapisha viungo vya mwili "BioPrinter". Inashangaza lakini ni wazo zuri, fikiria mfano unaenda hospitali na unahitajika ufanyiwe upasuaji wa figo, bila kusita wala kutafuta mtu wa kukupa figo yake, basi inaenda kuchukuliwa kutoka kwenye maabara tu. Kwa sasa watafiti kutoka vyuo vya Sydney, Harvard, Stanford na MIT wamefanikiwa kugundua uchapishaji wa mishipa ya damu hasa katika mapafu. Wametumia utafiti wao na njia mbali mbali za kitabibu hatimae wamefanikiwa kuchapisha mfumo wa mishipa midogo sana ya damu ndani ya mapafu. 

Chanzo: Engadget

Tuesday, July 01, 2014

CHINA KUJENGA JENGO LA 1KM KWA UREFU

China ipo katika mkakati wa ujenzi wa jengo refu kuliko yote duniani litakaloitwa ''Phoenix tower''. Jengo hilo linatarajiwa kumalizika kati ya mwaka 2017/2018 kuanzia ujenzi wake. jengo hilo litakalojengwa katika jimbo la  Hubei katikati mwa china linatarajiwa kuwa la kuvutia lenye rangi ya pink na litakuwa rafiki wa mazingira. Inategemewa jengo hilo litazidi jengo refu liliopo sasa la Buruj Khalifa kwa mita 172.
''Kutakuwa na mtaa wa Kifaransa, mtaa wa Kijapani, na hata mtaa wa Kituruki na mitaa mingine mingi zaidi amdayo itaruhusu watu kuiona dunia bila ya kuondoka China'' alisema Chetwood kuiambia ''The Guardian''. Mpaka sasa kuna ujenzi wa majengo mengi marefu yanayoshindana duniani ikiwemo Buruj Khalifa liliopo Dubai, na jingine ambalo ujenzi wake unategemewa kukamilika mwaka 2019 nchini Saudi Arabia litakaloitwa ''Kingdom tower'' na hili la nchini China.

Chanzo: CNN

 Hili ndo jengo refu kwa sasa la Buruj Khalifa huko Dubai


Hili ni jengo litakalo jengwa nchini Saudi Arabia litakaloitwa Kingdom Tower.





ISIS WATANGAZA UTAWALA WA KI-ISLAMU (KHILAFA)

Wapiganaji wa kiislamu wa Syria na Iraq watangaza dola ya kiislamu yaani Khilafa ikimaanisha mrejesho wa utawala huo uliomalizika takribani miaka 100 iliyopita baada ya kuanguka kwa utawala wa Ottoman. Kutokana na sauti zilizohifadhiwa na kusambazwa mtandaoni jumapili hii, utawala wa kiislamu wa Iraq  na ISIL wamethibitisha kuwa Kiongozi wao Abu Bakr Al-baghdadi kuwa ndio Khalifa wao na ndio kiongozi wa waislamu wa kila mahali. Baghdadi anaaminika kuwa kiongozi wa ISIL, ambayo ilijitangaza rasmi kuwa ni Taifa la kiislamu. Kutokana na maelezo yao, utawala huo mpya unaanzia nchini Iraq katika jimbo la Diyala mpaka Aleppo nchini Syria.
''Shura ya utawala wa kiislamu ilikutana na kujadili kuhusiana na utawala wa kiislamu. Hivyo utawala wa kiislamu uliamua kuanzisha khilafa na kumchagua khalifa wa waislamu wote'' aliarifu msemaji wa ISIL Abu Mohammad Al-Adnani.
''Majina ya 'Iraq' na 'the Levant' yameondolewa katika orodha ya taarifa muhimu ya utawala huo wa kiislamu'' alisema Adinani, akielezea kuwa utawala wa kiislam 'khilafa' ni ndoto ya waislamu wote na ni tumaini la wana-jihad wote. Inadhaniwa kuwa tangazo hilo linaweza kuleta mtafaruku kwa wapiganaji wengine wa kisunni nchini Iraq ambao wanapigana na serikali ya waziri mkuu Nour Al-Maliki na sio wanaopigana kwa ajili ya khilafa.

Chanzo: www.mwcnews.net

Thursday, June 26, 2014

MWANAFUNZI WA CHUO KUTOKA SAUDI ARABIA AUWAWA UINGEREZA


Inna Lillahi Wainna Ilayhi Raajiuun...........Nahid Almanea alikuwa ni mwanafunzi wa shahada ya pili  kutokea Saudi Arabia  wakati akiuwawa katika mashambulizi mabaya wiki iliyopita huko Colechestor, Essex nchini Uingereza. Msichana huyu alichomwa na kitu chenje ncha kali mara 16 katika mwili wake wakati akipita katika mitaa ya jiji hilo. Polisi bado wanaendelea na msako wa waliohusika na mashambulizi hayo. Tayari dada huyu ameshazikwa katika mji alikotoka wa Al-Jouf huko nchini saudi arabia na mazishi yake yalihudhuriwa na maelfu ya watu.

Nahid alikuwa miongoni mwa maelfu ya wanafuzi wanaosoma katika chuo cha Essex amabpo inakadiriwa kuna kama wanafunzi 22365 kutoka mashariki ya kati na 9440 ni kutoka Saudi Arabia. Kuna majadiliano mengi kuhusiana na kifo cha huyu dada lakini inasemekana mwanafuzi huyu alikuwa kavaa "hijab" na "abaya" hivyo kumfanya ajulikane kuwa ni muislamu. Polisi wanaendelea na uchunguzi lakini inadhaniwa huenda chuki dhidi ya uislamu ikawa ndio sababu kuu ya mauaji haya. vyombo vingi vya habari vya masharik ya kati vimeeleza kwa uwingi habari hii na wengi wao wanaamini ni kwasababu vyombo vya habari vya magharibi vimekuwa mstari wa bele kuuelezea uislamu kwa ubaya hivyo kuchangia chuki hizi dhidi  ya uislamu.  Cha kusikitisha ni kuwa vyombo vya habari vya magharibi havijaipa kipaumbele habari hii. 

Kifo cha Nahid Almanea ni cha kusikitisha ambacho kimepeleka huzuni kubwa katika familia yake. Huenda mashambulizi haya yakaongezeka maradufu ikiwa chuki dhidi ya uislamu na waislamu vitaachwa kuendelea kusambazwa hususan kupitia vyombo vya habari. matukio haya yatachangia kwa kiasi kikubwa waswasi miongoni mwa watalii na wawekezaji kutoka mashariki ya kati na pia kwa waislamu zaidi ya milioni 3 wanaoishi ndani ya Uingereza. 

Chanzo: www.middleeastmonitor.com


picha ya Nahid Almanea kwenye CCTV kabla ya kuuwawa


 
 maelfu ya watu kwenye mazishi ya marehemu Nahid Almanea mjini kwao huko Al-jouf




AL-QAEDA WASHAMBULIA UWANJA WA NDEGE WA YEMEN

Muda mfupi uliopita inasemekana wanamgambo wa Al-Qaeda wamehusika na shambulizi la uwanja wa ndege wa Yemen. Shambulizi limeathiri mnara wa kuongozea ndege, haya yamesemwa na viongozi wa ulinzi katika uwanja huo. Walinzi hao wanasema shambulizi hilo katika uwanja wa ndege wa Sayoun uliopo katika jimbo la kusini la mji wa Hadramawt lilanza kutoka maeneo matatu tofauti mapema Alhamisi ya leo.
Kutokana na shirika la utangazaji la AFP wanataarifu kuwa mpaka sasa wanajeshi watatu wameshafariki kutokana na shambulizi hilo japokwa kituo cha utangazaji cha aljazeera hawajathibitisha habari hizo. Inasemekana shambulizi hilo limetokea saa chache baada ya walinzi kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi katika mji huo unaojulikana kuwa miongoni mwa ngome kuu za wanamgambo wa Al-Qaeda.  

Chanzo: Al-Jazeera


Sunday, April 27, 2014

(SCHOLARSHIPS) NAFASI ZA KUSOMA NCHINI TURKEY!!!!

Je, unahitaji kwenda kusoma nchini Turkey? Bado hujapitwa, wahi sasa kwani wakati ndio huu. Turkey ni miongoni mwa nchi zilizoendelea duniani inayopatikana kati ya bara la Europe na Asia. Mpaka sasa kuna wanafunzi wengi sana kutoka nchi mbalimbali duniani wanaosoma nchini humo ikiwemo watanzania wengi wanaopatikana katika miji mbali mbali ya nchi hiyo kama Istanbul, Ankara, Izmir na miji mingine. Kuna vyuo vingi sana vya kisasa, hivyo serikali ya Uturuki imetoa nafasi nyingi sana (scholarships) katika vyuo vilivyopo nchini humo kwa wanafunzi wanaohitaji kwenda kusoma huko katika fani mbali mbali. Vipo vyuo vinavyotoa mafunzo kwa kituruki na vingine kwa kingereza. Lakini moja ya masharti yao ni lazima usome kituruki ukiwa mwanafunzi nchini humo. Lugha hii sio ngumu pindi utakapoingia darasani na kuisoma. Wapo wanafunzi wengi kutoka nchi mbali mbali wamejifunza na wanaijua vizuri lugha hii. Miongoni mwa huduma utakazopewa ni pamoja na ada ya shule, ticket ya kwenda na kurudi kutokea nchini mwako , hostel na mengine mengi. Kumbuka kabla ya kuchagua chuo, hakikisha kinatambuliwa na TCU ili usije pata matatizo pindi utakapomaliza masomo yako na kurudi Tanzania. Pia maombi yote yafanyike mtandaoni kupitia website halali iliyoidhinishwa na wizara ya nchi hiyo ambayo ni www.turkiyeburslari.gov.tr. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19/05/2014. Unaweza  kubofya hapa kutazama video ni jinsi gani ya kutuma maombi kwa urahisi. Kutokana na kuwa ni watu wengi duniani wanaofuatilia website hiyo inaweza kuwa inasumbua kufunguka kwa kipindi fulani, hivyo endelea kuifungua kila mara mpaka pale itakapokubali. Pia unaweza kufatilia taarifa zao za kila mara kupitia ukurasa wao wa Facebook hapaKILA LA KHERI!!!!!