Viongozi wa Israel wahusishwa na kifo cha Arafat
Mkuu wa Kamati ya Palestina inayochunguza kifo
cha Yassir Arafat amesema kuwa viongozi wa Israel walihusika kumuua kiongozi
huyo wa zamani wa Palestina. Tawfiq al Tirawi amesema ushahidi uliopo ni wa
matamshi yaliyotolewa na viongozi wa Israel waliosema kuwa Arafat lazima auawe
ambapo Shaul Mofaz na Ariel Sharon walifanya mazungumzo na kutaka kuuliwa
Arafat. Hivi karibuni Waziri wa Mawasiliano wa utawala wa Kizayuni alieleza kuwa
yoyote anayetaka kuchunguza kifo cha Yassir Arafat ajue kwamba kufanya hivyo ni
sawa na kutangaza vita na Israel. Mbali na waziri huyo, makumi ya maafisa wa
kisiasa, usalama na kijeshi wa utawala haramu wa Kizayuni walisema kuwa Arafat
ni lazima auliwe. Wapalestina wamekuwa wakisisitiza kwa miaka kadhaa sasa kuwa
Yassir Arafat aliuliwa kwa sumu na Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO