SUSAN RICE AKIRI ALIONGOPA KUHUSU KUUAWA BALOZI WA MAREKANI LIBYA
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice amekiri kwamba alitoa
taarifa ya uongo kuhusu matukio yaliyopelekea kuuawa balozi wa nchi yake huko
Libya miezi kadhaa iliyopita. Awali Rice alikuwa amesema shambulio dhidi ya
ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi, Libya lilikuwa la kigaidi lakini
mwishoni mwa wiki alikiri kwamba, waandamanaji wa Kiislamu waliokuwa na hasira
baada ya kuonyeshwa filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW ndio
waliovamia ubalozi huo na kuuchoma moto. Amesema Waislamu walikuwa na haki ya
kuonyesha hasira zao lakini akadai kwamba walichupa mipaka katika kuelezea
ghadhabu zao.
Matamshi ya Rice yamemuweka katika hali ngumu na Wabunge wa
upinzani wameapa kukabiliana na juhudi zozote za Rais Barack Obama za kumteua
kuwa Waziri wa Mambo ya Nje baadaye mwaka ujao. Rice alikuwa amepigiwa upatu
kuchukua nafasi ya Hillary Clinton anayemaliza muda wake mapema mwaka ujao.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO