Thursday, December 20, 2012

AFGHANISTAN WAKUTANA WA KUNDI LA TALIBAN

Maafisa wa serikali ya Afghanistan wanakutana na waasi wa Taliban na wajumbe wa kundi jengine moja la waasi karibu na Paris, wakitafuta namna ya kuumaliza uasi baada ya kujiondoa kwa vikosi vya kimataifa vilivyopo sasa Afghanistan. Wenyeji wa mazungumzo hayo, Ufaransa, imesema mkutano huo wa leo na kesho na ulio wa nadra sana kufanyika, hautarajiwi kujumuisha hila zozote kuelekea uwezekano wa kupata makubaliano ya amani. Zaidi wa wajumbe 20 kutoka serikali ya Rais Hamid Karzai, Taliban, vyama vya upinzani na wale wa kundi la Hizbul-Islam watajaribu kufanya mazungumzo baada ya miaka 11 ya vita. Mkutano huo unafanyika katika wakati ambapo Ufaransa inajitayarisha kuondoa wanajeshi wake wa mwisho kutoka Afghanistan, kabla ya tarehe ya kuondoka kwa vikosi vya jumuiya ya kujihami ya NATO. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO