Thursday, December 20, 2012

UN NAO YAIONYA SERIKALI YA LEBANON

Umoja wa Mataifa umeionya Lebanon kuwa raia wake wanaopigana vita nchini Syria wanaiweka nchi yao katika hatari ya kuingizwa kwenye mzozo huo. Mkuu wa Masuala ya siasa katika umoja huo Jeffrey Feltman amesema kuwa kuna ripoti nyingi zinazoonyesha kuwa raia wa Lebanon wanapigana katika upande wa Rais Bashar al Assad nchini Syria. Vitendo hivi vya raia wa nchini hiyo kuusaidia utawala nchini Syria vinakiuka sera ya nchi hiyo ya kutokujihusisha na mzozo wa Syria. Serikali dhaifu ya Lebanon ilishaamua kujiweka mbali na mzozo wa Syria wakati kukiwa na mgawanyiko kuhusu uasi wa nchi hiyo. Pamoja na onyo hilo Umoja wa Mataifa umeelezea pia wasiwasi wake juu ya kuongezeka shughuli za kijeshi kwenye eneo la milima ya Golani ambalo ni ukanda maalumu usioruhusu shughuli hizo baina ya Syria na Israel. Kuongzeka kwa shughuli za kijeshi katika eneo hilo kunatishia pia kuongezeka kwa mzozo wa Syria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO