Saturday, December 22, 2012

NETANYAHU AIPUUZA UN

Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni amesema kuwa hajali kuhusu kile kinachosemwa na Umoja wa Mataifa kuhusu mpango ya Tel Aviv wa kutaka kujenga vitongoji zaidi vya walowezi wa Kiyahudi akiahidi kuwa Israel itaendeleza ujenzi huo. Netanyahu ametoa matamshi hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na kanali nambari mbili ya Israel hapo jana. Mahojiano kamili ya Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni yamepangwa kutangazwa leo Jumamosi. Benjamin Netanyahu amedai kuwa al Quds ni mji mkuu wa Israel na wala si ardhi iliyoghusubiwa na kwamba hajali kile kinachosemwa na Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO