Maharamia 11 wa Kisomali ambao walishambulia meli ya kubeba mafuta ya Italia mwezi Januari mwaka huu wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu na nusu jela kila mmoja baada ya mahakama ya Roma kuwapata na hatia ya uharamia na jaribio la utekaji nyara.
Imearifiwa kuwa maharamia hao walishambulia meli hiyo ya mafuta ijulikanayo kama Valdarno yapata maili 250 kutoka pwani ya Yemen lakini wakashindwa nguvu na jeshi la wanamaji la Italia ambalo lilikuwa likilinda doria katika eneo hilo.
Katika miaka ya hivi karibuni maharamia katika Bahari ya Hindi wamekuwa wakishambulia meli za kimataifa na kupata mamilioni ya dola kama kikomboleo kabla ya kuachilia huru mabahari na meli walizofanikiwa kuziteka nyara.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO