Nchini Somalia askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika pamoja na wanajeshi
wa Somalia wameuteka mji wa Jowhar kutoka wapiganaji wa Kiislamu, al Shabaab. Mkaazi mmoja alisema wanajeshi hao waliingia
bila ya pingamizi. Kupoteza
mji wa Jowhar ni pigo kubwa kwa al-Shabaab.
Mji huo uko kilomita 90 kaskazini
ya Mogadishu, kwenye barabara kuu ya Somalia inayounganisha majimbo ya kusini
na kati. Piya uko katikati ya eneo la kilimo kikubwa cha nchi. Jowhar ilikuwa
ikidhibitiwa na al-Shabaab tangu wanajeshi wa Ethiopia walipoondoka Somalia
mwaka wa 2009. Ulikuwa mmoja kati ya miji mikubwa iliyokuwa bado mikononi mwa
al-Shabaab.
Tangu mwaka 2011
al-Shabaab imepoteza makambi yake kadha.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO