Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Mazungumzo hayo yamefanyika Cairo Jumatano ya leo pembizoni mwa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC). Mahmoud Abbas na Rais Ahmadinejad wamejadili kadhia ya Wapalestina na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.
Katika kikao hicho Rais Ahmadinejad amesema katika kipindi cha miaka 34 iliyopita, Iran haijabadilisha msimamo wake imara wa kuwaunga mkono Wapalestina. Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio nchi pekee ambayo kamwe haijawahi kuutambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema Iran inaamini Wazayuni ni maghasibu ambao waliingia katika eneo hilo kwa mabavu na kukanyaga haki za Wapalestina.
Kikao cha siku mbili cha viongozi wa nchi 57 za OIC kimeanza leo Februari 6 mjini Cairo. Rais Ahmadinejad wa Iran pamoja na viongozi wengine wanaoshiriki wanajadili matatizzo ya ulimwengu wa Kiislamu hasa njia za kutatua mgogoro wa Syria, kadhia ya Palestina na vita nchini Mali.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO