Duru za habari kutoka Afghanistan zinaarifu kuwa, wanajeshi wanane wa Shirika la
Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO wameuawa katika mripuko uliotokea karibu na
uwanja wa ndege wa Kandahar nchini Afghanistan. Jana wapiganaji wa kundi la
Taliban walitangaza kuwa, bomu walilokuwa wamelitega karibu na uwanja huo,
liliwaua wanajeshi wanane wa kigeni. Aidha Taliban wamesisitiza kuwa, bomu hilo
liliripuka kando ya barabara wakati msafara wa vikosi vya NATO ulipokuwa ukipita
katika barabara hiyo. Wengi wa waliouawa katika mripuko huo ni askari wa
Marekani na Uingereza.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO