Kaimu Waziri wa Habari nchini Pakistan,
amesisitizia udharura wa kufutwa vikwazo vya Wamagharibi dhidi ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran. Rashid Ahmad Chaudhri aliyasema hayo katika mahojiano na
waandishi wa habari mjini Islamabad, Pakistan, na kusisitiza kuwa, nchi yake
inawataka Wamagharibi kufutilia mbali vikwazo walivyoiwekea Tehran kwa
kisingizio cha sialaha za nyuklia na kwamba Islam Abad inapinga mbinyo wa
baadhi ya nchi za kibeberu dhidi ya nchi nyengine kwa kisingizio cha matumizi ya
silaha za nyuklia.
Kiongozi huyo wa Pakistan pia amezungumzia makubaliano ya
Tehran na Islamabad kwa ajili ya kuanza utekelezwaji wa ujenzi wa bomba la amani
la usafirishaji gesi kutoka hapa nchini hadi Pakistan na kuongeza kuwa, Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran ni nchi ya kwanza kusafirisha gesi kwenda Pakistan na kwamba
nchi yake ina hamu ya kuona uhusiano wa nchi mbili unaimarishwa zaidi hasa
katika sekta za nishati.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO