Wizara ya Ulinzi ya Yemen imetangaza kuwa,
maafisa usalama wa nchi hiyo wamefanikiwa kukamata lori lililosheheni silaha
ambazo inasaidikiwa kuwa zimetengenezwa nchini Uturuki. Gari hilo lilikamatwa
karibu na bandari ya Al-Hodayda iliyoko katika pwani ya magharibi mwa Bahari
Nyekundu nchini Yemen. Maafisa hao wa usalama wa Yemen wamesisitiza kuwa, silaha
hizo za Uturuki zilikuwa katika maboksi na makatuni ya plastiki pamoja na bidhaa
za aina nyingine zilizokuwemo ndani ya gari hilo na kwamba gari hilo
lilisimamishwa na maafisa hao katika eneo la pwani yapata kilomita 30 kutoka
katika bandari hiyo ya Al- Hodayda nchini Yemen. Itakumbukwa kuwa, mwezi
uliopita kulienea habari ya kukamatwa gari lililokuwa limebeba silaha za Uturuki
katika bandari ya Aden kusini mwa Yemen. Tayari maafisa hao wa usalama
wametangaza kuanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO