Sunday, December 23, 2012

BALOZI WA MAREKANI AFUKUZWA, KATIBA YAPITA

Wananchi wenye hasira wa Misri wamemfukuza balozi wa Marekani katika kituo kimoja cha kupigia kura huku akisema kwa sauti kubwa: "Tunataka Uislamu." Mwandishi wa kanali ya kwanza ya televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameripoti habari hiyo kutoka mjini Cairo na kuongeza kuwa Anne W Patterson, Balozi wa Marekani mjini Cairo alilazimika kuondoka kituoni hapo baada ya kuona kuona hasira hizo za wananchi wa Misri. Wakati huo huo asilimia 70 ya wananchi wa Misri walioshiriki kwenye awamu ya pili ya kura ya maoni wameunga mkono rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo. 
Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri leo imetoa matokeo ya awali ya awamu ya pili na ya mwisho ya kura ya maoni kuhusu katiba hiyo mpya. Ikhwanul Muslimin imesema kuwa jumla ya asilimia 64 ya wapiga kura huko Misri wameipigia kura ya ndio rasimu hiyo. Chama cha Uhuru na Uadilifu ambacho ni tawi la kisiasa la harakati ya Ikhwanul Muslimin kimeeleza kuwa wananchi wa Misri wameendeleza mchakato wa kujenga demokrasia bora nchini mwao. Wamisri zaidi ya milioni nane kati ya raia milioni 25 wanaostahiki kupiga kura walipiga kura zao kwenye mikoa 17 ya Misri katika awamu ya pili ya kura ya maoni kuhusu rasimu hiyo. Rasimu  hiyo inaeleza kuwa marejeo makuu ya katiba ya Misri itakuwa ni dini tukufu ya Kiislamu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO