Sunday, December 23, 2012

TALIBAN WAUWA WANAJESHI KUMI WA MAREKANI

Kundi la wanamgambo wa Taliban la Afghanistan limesema kuwa limewauwa wanajeshi vamizi wa Marekani wasiopungua kumi katika shambulio walilofanya dhidi ya msafara wa vikosi vya Marekani katika mkoa wa Nangarhar huko mashariki mwa Afghanistan. 

Wanamgambo wa Taliban leo waliushambulia msafara wa wanajeshi vamizi wa Marekani wakati wanajeshi hao walipokuwa wakivuka katika kivuko cha Torkham kati ya Pakistan na Afghanistan wakielekea Jalalabad mkoani Nangarhar. Habari zinasema kuwa ufyatulianaji risasi ulijiri kati ya pande mbili hizo, na kudumu kwa saa moja. Raia watatu waliuliwa pia katika ufyatulianaji risasi huo kati ya Taliban na vikosi vamizi vya Marekani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO